demashole

Sengo

BRUCE

Thursday, August 21, 2014

Marekani yaishambulia IS licha ya onyo

Bwawa la Mosul lililotekwa kutoka kwa wapiganaji wa IS
Majeshi ya Marekani yameendelea kuwashambulia wapiganaji wa Islamic State huko Iraq licha ya vitisho kutoka kwa kundi hilo kuwa watawaua mateka wengine wamarekani iwapo Obama angeendelea kuishambulia himaya hiyo kaskazini mwa Iraq.

RATIBA LIGI KUU YATOKA; YANGA SC KUANZA NA MTIBWA SUGAR MOROGORO, AZAM NA POLISI MORO, SIMBA NA COASTAL DAR

Kocha wa Yanga SC, Marcio Maximo akiwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Mbrazil mwenzaje Jaja. Timu yao itaanzia Ligi Kuu ugenini na Mtibwa Sugar

  -------------------------
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM(bongostaz.blogspot.com)
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wataanza na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Septemba 20, mwaka huu, wakati Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo.

Wahanga ndege ya Malaysia waibiwa fedha

Ndege ya shirika la ndege ya malaysia wakati wa uhai wake.
Ofisa mmoja mwanamke mwenye cheo cha juu katika bank kubwa iliyoko mjini Kuala Lumpur , Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba mamilioni ya dola za kimarekani kutoka katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege iliyopotea ya Malaysia Air Line MH370 ambayo ilipotea katika mazingira ya kutatanisha,katika bahari ya Hindi mapema mwezi March.

KIBOKO CHA MAN U, SWANSEA CITY WASAJILI BEKI LA ARGENTINA KOMBE LA DUNIA

Uhakika: Federico Fernandez akiwa ameshika jezi ya Swansea City baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 8 kutoka Napoli

HABARI ZILIZOTUFIUKIA HIVI PUNDE ; DAKTARI MSTAAFU WA HOSPITAL YA PERAMIHO AJINYONGA

http://www.inkamana.org/images/perahosp.jpg
Katika hali isyokua ya kawaida aliyewahi kuwa Daktari katika Hospitali ya Mtakatifu JOSEPH ya PERAMIHO Dr FREDRICK MGAYA amejinyonga kando ya uwanja wa michezo wa Abasia ya PERAMIHO SONGEA VIJIJINI.

WAHAMIAJI HARAMU 21 WALIOKAMATWA MKOA WA NJOMBE WAREJESHWA NCHINI KWAO

 Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa NJOMBE ROSE MHAGAMA 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA AMEANZA KUTOA ELIMU YA POLISI JAMII

http://4.bp.blogspot.com/-wfXXzFHZCZ4/U9IhnUPZlKI/AAAAAAAAJRA/BTiepDyP7cQ/s1600/DSC02590.JPG
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa RUVUMA MIHAYO MSIKHELA ameanza kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya ulinzi kwa lengo la kuimarisha Program ya Polisi Jamii inayolenga kuwahusisha wana jamii katika ulinzi.

Alhaj Ali Hassan Mwinyi asema bado viongozi wanatumia madaraka yao kujinufaisha

Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma. Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.

MSAADA TUTANI,,,NYUMBA HIZI ZINAPANGISHWA KWA AJILI YA BIASHARA YA HOTELI KATIKA MKOA MPYA WA NJOMBEMkoa mpya wa njombe unaokua kwa kasi kubwa na kuibua  fursa nyingi  za biashara ya  kila aina sasa unaweza kuanza biashara ya hoteli kwa kupangishwa tu moja ya majengo haya  yaliyo tayari kwa biashara hii  kwanza kwa kuwa eneo lenye mzunguko wa watu na pia kuweza kutimiza malengo yako kwa  wakati

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014.

MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AUNDA KAMATI NDOGO

mkiti 1
Na Magreth Kinabo, Dodoma  
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameunda kamati ndogo yenye ujumbe wa watu 10 kwa ajili ya kushughulikia masuala ambayo  hayakufikia muafaka wakati wa majadiliano ya kupitia sura mbalimbali za Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Kamati 12 za Bunge hilo.

MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMTI KUU MJINI DODOMA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM Dodoma.
-----------
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi alisema, Kamati Kuu pamoja na mambo mengine, ilipokea taarifa na kufanya tathimini juu ya maendeleo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini, ndani na nje ya Bunge.

VIONGOZI WA TANZANIA WATEMBELEA KITUO CHA MAZINGIRA FINLAND

 Mtaalam wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kutoka kituo cha mazingira cha Finland akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa Tanzania kuhusu htu zinazochukuliwa na nchi hiyo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Wednesday, August 20, 2014

TANZANIA YAPOKEA MWONGOZO MPYA WA SHERIA NA KANUNI ZA HAKI ZA BINADAMU

IMG_0389 
Mtendaji Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay akifungua Warsha ya siku mbili juu ya mwongozo mpya wa Sheria na Kanuni za polisi kumweka mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla ya kusikilizwa.warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam jana (leo).

EBOLA:POLISI WAVUNJA MAANDAMANO LIBERIA

 
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf atangaza amri ya kutotoka nje .
Maafisa wa usalama wakiwa Westpoint baada ya uvamizi wa kituo cha Ebola
Polisi nchini Liberia wamerusha vitoa machozi kuwatawanya umati uliojaa hasiria katika mji mkuu Monrovia wakipinga kuzingirwa kwa kitongoji chao na maafisa wa Usalama.

MAGAVANA WA BENKI YA PTA KUKUTANA TANZANIA

01 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (katikati) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Dodoma juu ya mkutano wa 30 utakaofanyika      nchini mwishoni wiki hii. Kushoto ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.

SERIKALI INAJENGA KIWANDA CHA KUZALISHA VIUADUDU VYA VILUWILUWI VYA MBU

Meneja uhusiano wa shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Bw, Abel Ngapemba akiongea na wanahabari ambao (hawapo pichani)
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kutumia Euro Milioni 16 katika ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vinavyoua viluwiluwi vya mbu wanaoambukiza malaria ulioko chini ya shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

SHTUMA KUFUATIA MAUAJI YA MWANDISHI

Picha kutoka kwa kanda hiyo ya video ya James kabla ya kuuawa
Kumekuwa na shutuma za kimataIfa kufuatia kuuawa ukatili kwa mwandishi wa habari raia wa Marekani na kundi la islamic state nchini Syria.

MWINYI,SERIKALI HAIKUFUTA AZIMIO LA ARUSHA

4488510_orig
Na Joseph Ishengoma
MAELEZO
Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema serikali haijawahi kufuta Azimio la Arusha kama inavyodaiwa na baadhi ya wananchi, bali ilizimua azimio hilo kuwapatia viongozi wa kati uwezo wa kumudu makali ya maisha.

BASI LA SKYLINE LINALOFANYA SAFARI ZAKE KATI YA MBEYA NA DODOMA LAPINDUK MLIMA NYOKA

 Askari wa Usalama Barabarani akikagua basi la Skyline lililopinduka leo katika Mlima Nyoka na hakuna aliyeripotiwa Kupoteza maisha katika ajali hiyo

TAARIFA KWA WABUNGE NA WAGOMBEA WATARAJIWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2015 TANZANIA

Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais unataraji kufanyika hapo mwakani, Wabunge na wanaotaka kuwania Ubunge katika majimbo mbalimbali nchini hata urais mnakaribishwa kuandaa TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA VYAMA VYENU. Kitabu kama hicho kitakuwezesha wewe Mgombea kuto tumia nguvu kuubwa ya kujinadi badala yake utavigawa kwa wananchi mbalimbali jimboni kwako nawe kuelewa nini umewafanyia katika kipindi ambacho ulikuwa madarakani. 

KIKWETE AKABIDHI TUZO BRN MBINGA *CHAKULA CHA MCHANA CHAPANDISHA TAALUMA.


http://2.bp.blogspot.com/-QE3jUF7g27Y/UcGoAUb389I/AAAAAAAAA9s/x1afDlVkF6A/s1600/E85A4252.JPG

Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la saba kutoka kata ya Kigonsera Kilayani Mbinga wakipata chakula cha mchana.(Picha na Maktaba)

UONGOZI WA MAJI MAJI WAWATAHADHARISHA WANAONYEMELEA WACHEZAJI WA TIMU HIYO

 Mwenyekiti wa klabu ya Maji Maji Humprey Milanzi
--------------------------------
Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
WAKATI usajili ya wachezaji kwa ajili ya kushiriki mashindano ya ligi kuu Tanzania bara na ligi daraja la kwanza ukiendelea uongozi wa klabu ya Maji maji ya mjini Songea mkoani Ruvuma maarufu kama Wanalizombe umevitatahadharisha vilabu ambavyo vimeonesha kuwanyemelea wachezaji wa timu ya Maji maji kwa kuvitaka kufuata taratibu za kuwachukua wachezaji wake.

MKUU WA MAJESHI TANZANIA JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE AFUNGUA KIWANJA KIPYA CHA MICHEZO ZANZIBAR.

01
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akipokea saluti mara baada ya kuwasili kwenye  ufunguzi wa kiwanja kipya cha Michezo kilichopo Makao Makuu ya Brigedi ya Nyuki Migombani.

Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete aongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dodoma

 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Kulia ni Makamu wa CCM (Bara) Ndg Philip Mangula akifuatiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana

NEW MUSIC: MPAKA KUCHEE - CHIDD BENZ FT DIAMOND & AY [AUDIO].

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atuma Salamu za Rambirambi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

jm1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.PICHA NA IKULU

Serikali kulipia wanafunzi wa sayansi wapatao 5000 ngazi ya stashahada mwaka wa masomo 2014/15


Mkurugenzi-Msaidizi-wa-Habari-Elimu-na-Mawasiliano-wa-Bodi-ya-mikopo-Tanzania-Cosmas-Mwaisobwa.
NA SULEIMAN MSUYA
KATIKA juhudi za Serikali za kukabiliana na upungufu wa uchache wa waalimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwenye shule mbalimbali za msingi na sekondari hapa nchini imesema italipia wanafunzi wapatao 5000 wa ngazi ya stashahada katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa mwaka wa masomo 2014/15.

MAMBO YAIVA ZIARA YA REAL MADRID NCHINI… FIGO, OWEN NA KAREMEBU WATUA KESHO DAR

 
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM(Kwa hisani ya bongostaz.blogspot.com)
MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Mreno Luis Filipe Madeira Caeiro Figo anatarajiwa kutua kesho na msafara wa kwanza ya magwiji wa Real Madrid tayari kwa mchezo dhidi ya magwiji wa Tanzania Agosti 23 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  

Figo ataongozana na nyota wengine wawili waliowika Real Madrid muongo uliopita, mshambuliaji Michael Owen aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi Kombe la Dunia mwaka 1998 Ufaransa na mwanasoka bora wa Oceania mara mbili 1995 na 1998 Christian Karembeu.

Figo aliyestaafu Mei 31 mwaka 2009, alipiga tuzo mbili mfululizo mwaka 2000, Mwanasoka Bora Ulaya na Dunia na anakuja Tanzania kuwakumbushia watu enzi zake anatamba Real Madrid.
Figo anatua kesho Dar es Salaam

JE AZAMU FC LEO WATATOKA KWA EL MERREIKH YA SUDAN ?

 AZAM FC
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kagame Cup, Azam FC watakuwa uwanjani jioni ya leo kuwakabili timu ya El Merreikh ya Sudan Kaskazini katik  mchezo wa robo fainali ya tatu.

Patrick Omog, kocha wa Azam FC tayari ameshafanya maandalizi muhimu kuelekea mchezo wao war obo fainali dhidi ya timu bora ya Merreikh ambayo imeshinda mchezo mmoja tu kati ya mitatu ya hatua ya makundi.

Tuesday, August 19, 2014

AJALI MBAYA YATOKEA MKOANI TABORA BAADA YA MABASI YA SABENA NA A.M. DREAMLINE KUGONGANA USO KWA USO.

 Watu zaidi ya watano wanasadikika kufariki dunia hii leo majira ya alasili leo katika ajali iliyotokea eneo la Mkolye, takribani km 4 toka Mjini Sikonge baada ya basi la Sabena lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Mwanza na basi la A.M. toka Tabora kwenda Katavi kugongana uso kwa uso. 

Kuhusu wale watoto wawili waliomuua kwa kumnyonga mwenzao wa miaka mitatu Manyara

Screen Shot 2014-08-19 at 1.09.12 PM 
Kuna ile stori ya Watoto wawili mmoja miaka 10 na mwingine 7 wote kutoka wilayani Hanang mkoani Manyara ambao walikua wanatuhumiwa kumuua mwenzao wa miaka mitatu kwa kumchapa na kisha kumnyonga, ilikua taarifa kubwa sana ndani ya wiki nne zilizopita.

Taarifa Kwa Umma Kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kuhusu Udhibiti wa Vyakula Vilivyoongezwa Virutubishi


Napenda kwa heshima na taadhima kutumia fursa hii kwa niaba ya Menejimenti ya TFDA na wafanyakazi wote kwa ujumla kuwakaribisha katika mkutano huu.  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo imeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura ya 219. Pamoja na mambo mengine, TFDA imepewa jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti usalama wa vyakula.

APR YAITOA KWA MATUTA RAYON, KUKUTANA NA POLISI YA RWANDA PIA NUSU FAINALI, KAZI IPO KESHO AZAM NA MERREIKH NYAMIRAMBO

Mugiraneza Jean Baptiste akishangilia baada ya kufunga penalti ya ushindi ya APR 


 Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI
POLISI na APR, zote za Rwanda zimekwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuwatoa wapinzani wao, Atletico ya Burundi na Rayon Sport pia ya Rwanda kwa penalti.
Baada ya sare ya bila kufungana baina yao na Atletico ndani ya dakika 90, Polisi ilikwenda kushinda kwa penalti 9-8, wachezaji wote 22 wakipiga hadi makipa.


Diwani Sagamiko aandaa warsha kwa wenyeviti na makatibu UWT Kinondoni

Kuluthum Sagamiko akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo  .